HabariSiasa

Mtoto wa Museveni apandishwa cheo baada ya kauli zake tata mtandaoni

Mtoto wa rais wa Uganda, Muhoozi Kainerugaba, ameondolewa katika wadhifa wake kama kamanda wa majeshi ya nchi kavu nchini humo.

Hata hivyo alipandishwa cheo hadi kuwa jenerali kamili, cheo cha juu zaidi katika jeshi. Anasalia kuwa mshauri wa rais katika shughuli maalum.

Haijabainika ikiwa uamuzi huu una uhusiano wowote na msururu wa ujumbe wa Twitter wenye utata katika siku mbili zilizopita.

Jenerali Kainerugaba hapo awali alikuwa kamanda wa kikosi maalum ambacho kinasimamia ulinzi wa Rais Yoweri Museveni.

Jenerali Kayanja Muhanga, ambaye ameongoza oparesheni ya jeshi la Uganda nchini Somalia na kwa sasa anaongoza kikosi kinachopigana na waasi wa Allied Democratic Front (ADF) nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, atachukua nafasi ya kamanda wa vikosi vya nchi kavu.

Siku ya Jumatatu, Jenerali Kainerugaba aliandika kwenye Twitter kwamba itamchukua yeye na jeshi lake wiki mbili tu kuchukua mji mkuu wa Kenya Nairobi.

Lakini asubuhi ya Jumanne, alisema kuwa alizungumza na babake, Rais Museveni, na kukiri kwamba tweets zake zilizua taharuki nchini Kenya.

Aliongeza kuwa rais “atatangaza mabadiliko”, ingawa hakuweka wazi hili ikiwa anarejelea mabadiliko katika jeshi.

Serikali ya Uganda imejitenga na mjadala wa mitandao ya kijamii ulioibuliwa na msururu wa ujumbe wa Twitter kutoka kwa mtoto wa rais.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents