Habari

Mtuombee kwaajili ya watu wasiojulikana – Mhe. Nassari

Mbunge wa Arumeru, Joshua Nassari baada ya Mbunge wa Iringa Mjini kumaliza kuzungumza na waandishi wa habari ameomba waandishi wawaombee kwaajili ya watu wasiojulikana.

Akizungumza leo nje ya Ofisi za TAKUKURU, Mhe. Nassari amesema neno hilo huku waandishi wa habari wakicheka na kutawanyika nje ya ofisi hizo.

Katika hatua nyingine, mara tu alipotoka nje ya ofisi hizo amesema kuwa amemuahidi Mkurugenzi wa Taasisi hiyo kuwa baada ya kufungua jalada atamletea ushahidi wote aliokuwa nao.

“Tumekutana na Mkurugenzi wa TAKUKURU, Ndugu Valentino Mlowola yeye pamoja na timu yake akiwemo mkurugenzi wa investigation tumekubaliana mambo mengi sana ya msingi kwanza kabisa tuiwadhibitishie Watanzania kuwa umeanza rasmi kwa suala la ununuzi wa madiwani ambalo sisi tunaushahidi usiotia shaka walikuwa hawajiuzulu kumuunga mkono Rais bali walikuwa bali walikuwa wanajiuzulu kuunga mkono Rushwa uchunguzi umeanza rasmi,” amesema Mhe. Nassari.

“Lakini ili jalada liweze kufunguliwa inabidi nije siku ya kesho au wakati ntakao naona unafaa ili niweze kuandika malalamiko yangu rasmi ili niweze kushirikiano kwenye uchunguzi wa suala ili lakini nimekabidhi ile flash nilio ikabidhi kwa waandishi wa habari ila hii nimeiongeza kidogo na nimemuhakikishia Mkurugenzi kwamba tutakavyo fungua jalada ntamletea ushahidi ambao niko nao kwahiyo kwa hatua za awali tumepokelewa vizuri.”

Mbunge wa Arumeru, Joshua Nassari na Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema wana watuhumu CCM kuwanunua wabunge wa Chadema ambapo leo wamewasilisha ushahidi wa awali.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents