HabariMichezo

Mwakinyo afunguliwa, amshukuru Rais Samia, Waziri Ndumbaro

Kamisheni ya kusimamia ngumi za kulipwa Tanzania (TPBRC), imemuondolea adhabu Bondia Hassan Mwakinyo na sasa yupo huru.

Mwakinyo alifungiwa mwaka mmoja na faini ya Milioni moja kwa kushindwa kupanda ulingoni kwenye pambano lake la Septemba 29 dhidi ya Bondia kutoka Namibia, Julius Indongo.

Champez aligoma kuingia ulingoni akidai kuwa waandaaji wa pambano hilo walienda kinyume na makubaliano.

”Awali ya kumshukuru allah tabaraqah wa ta’ala kunijaalia Hekma, uvumilvu busara nyakati zote pamoja na subra kwa mashabiki wangu napenda kuushukuru Umma na wafuasi wangu wote niishukuru serekali ya MAMA samia kupitia Baraza la michezo la taifa chini ya Mh wazir Ndumbaro pamoja na naibu wazir kwa kusimamia haki na usawa wa wana michezo I can’t wait to show quality boxing high skills and ring iq 🤗🤗 wasena this era is Coloradoking era… shout out for all mogadishu family,”- Ameandika Hassan Mwakinyo

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents