Burudani

Mwenye uwezo wa kupambana na Diamond ni Alikiba – Edu Boy

Msanii wa muziki wa hip hop Bongo, Edu amefunguka undani wa mistari ambayo inapatikana katika ngoma yake mpya ‘Tunasafisha’.

Rapper huyo ambaye katika ngoma hiyo amewachana wasanii kadhaa wakubwa Bongo ameiambia The Playlist ya Times Fm kuwa mwenye uwezo wa kushindana na Diamond kimuziki ni Alikiba na sio Ommy Dimpoz kama alivyochana.

“Mtu mwenye uwezo wa kupambana naye (Diamond) ni Alikiba ila kwa Ommy Dimpoz bado sana,” amesema.

“Ukiangalia hapo katikati kulikuwa na beef mtandaoni zilikuwa zinaendelea sijui kama ni za kibiashara au vipi, watu wakawa wanawashindanisha ila inaonekana Dimpoz kalemewa ila ikitokea kwa Kiba na Diamond unaona huu ni mpambano,” amesisitiza.

Katika ngoma hiyo kuna mstari unasema; Simba wa sasa hana madhara sana, labda Tembo kwa Dimpoz kupambana jipange sana/

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents