HabariMichezo

Mzee Mwinyi atimiza miaka 98, Rais Samia amtakia kheri

Rais Samia Suluhu Hassan amemtakia kheri Rais Mstaafu wa awamu ya Pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi anapotimiza umri wa miaka 98.

”Nakutakia kheri mzee wetu na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi unapotimiza umri wa miaka 98. Tunaendelea kukushukuru kwa utumishi wako kwa nchi yetu na busara zako. Nakuombea Mwenyezi Mungu aendelee kukukirimia neema zake, akujalie furaha na siha njema.”- Samia Suluhu Hassan

Mzee Mwinyi alizaliwa Mei 8, 1925 huko mkoani Pwani na alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia mwaka 1985 hadi mwaka 1995.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents