Burudani

Namuonea huruma Diva, namwombea kwa Mungu amrudishie akili zake! – Ruby

Baada ya mtangazaji wa Clouds FM, Diva kudai kwamba hamjui msanii wa muziki Ruby, Ruby ameendelea kutema cheche kuhusiana na kauli hiyo.
ruby-na-diva

Muimbaji huyo ambaye ameachana na uongozi wake wa zamani wa THT, ameonyesha kuchukizwa na kauli hiyo ya Diva ambapo kila akiulizwa kuhusu kauli hiyo amekuwa akitoa maneno makali.

“Kuhusu Diva, bora tu niachane naye maana sioni vitu vya kumuongelea kama anavyofanya yeye,” Ruby aliliambia gazeti la Mtanzania “Zaidi namuonea huruma tu, namsikitikia na ninamwombea kwa Mungu amrudishie akili zake. Nahisi ana ugonjwa wa kusahau, jambo ambalo ni baya sana kulingana na umri wake,”

Pia muimbaji huyo amesema kwa sasa amefunga ukurasa wa kuzungumzia masuala ya uongozi wake uliopita huku akidai kwa sasa ana nafasi ya kufanya vizuri zaidi kimuziki akiwa mwenyewe.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents