Burudani

Nash MC awataka wasanii kupinga matumizi ya dawa za kulevya

Rapper Nash MC amewataka wasanii pamoja na wadau mbalimbali kupaza sauti zao katika kupinga matumizi ya dawa za kulevya.

11848904_877838228930484_1428645358_n

Akizungumza kwenye kipindi cha Harakati cha Clouds TV kinachoendeshwa na Kalapina, Nash alisema kila mtu ana jukumu la kuelimisha vijana kuhusu matumizi ya dawa za kulevya.

11363936_476611919163878_1291724406_n
Nash MC pamoja na Kalapina wakiwa katika harakati za kuelimisha jamii

“Baadhi ya wasanii wenzetu wengi wameingia huko, wengine wamefariki tumewazika, wengine marafiki zetu wa karibu tumewazika kitu ambacho kinauma kabisa,” alisema. “Hata jamii inafahamu kuna wasanii wenzetu wengi wamefariki kwa madawa ya kulevya. Mimi nimekuwa nikitumia muda mrefu kuongelea suala hili na kuwataka wasanii pamoja na wadau mbalimbali kuelimisha jamii juu ya athari za matumizi ya madawa ya kulevya.”

“Ndio maana pia nilimpigia Kalapina ili tuje tuzungumze na watu wa Temeke walioingia kwenye tatizo hili,” alisisitiza Nash.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents