Technology

WhatsApp yaongeza features mpya ikiwemo ‘emoji’ ya kidole cha kati!

WhatsApp imeboresha zaidi huduma zake kwa kuongeza baadhi ya vitu ambavyo havikuwepo katika matoleo yaliyopita. Maboresho hayo ni kwa watumiaji simu za Android.

whatsapp-1

Katika version mpya 2.12.250, sasa mtumiaji wa WhatsApp anaweza ku-customize notifications kwa mtu mmoja mmoja au kwa kila kundi alilonalo, ikiwemo vibration length, popup notification, notification light na call notification tone.

Whatsapp2

Kingine anaweza kusoma ujumbe na kuurudisha uonekane haujasomwa au umesomwa kwa kubonyeza kwa muda mrefu bila kuachia chati husika.

Whatsapp3

Katika version mpya pia zimeongezwa ‘emoji’ mpya ikiwemo ya ‘kidole cha kati’.

Update hiyo sasa inapatikana kwenye Google Play Store.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents