Burudani

Nay asema wimbo ‘Saka Hela’ utawafanya vijana kuingia mzigoni kusaka pesa

Rapa Nay wa Mitego baada ya kufanya vizuri na wimbo ‘Shika Adabu Yako’, Jumatatu ijayo anatarajia kuachia wimbo mpya uitwao ‘Saka Hela’.
Nay

Akizungumza na Bongo5 hivi karibuni, Nay amesema mara nyingi amekuwa akionyesha mali zake pamoja na pesa ili kuwatia machugu vijana ya kutafuta pesa.

“Tarehe 9 ya mwezi huu, i mean Jumatatu ijayo nitaachia rasmi video yangu mpya ya ‪wimbo ‘SakaHela’ , ‬ kaa tayari kwenye runinga yako. Saka Hela ni wimbo ambao unatoa majibu kwanini mara nyingi nimekuwa nikionesha mali zangu, kwa hiyo mashabiki wakae mkao wa kula kuona kigongo kingine,” alisema Nay.

Nay ni mmoja kati ya wasanii ambao wanaweza kucheza na hisia za mashabiki wake kutokana namna ya utunzi wa mashairi yake ambayo huwashika mashabiki.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents