Fahamu

Nchi hizi 10 zinazongoza kwa rushwa duniani

Kwa mujibu wa Jarida la Forbes na Takwimu za Transparency International, hizi ndizo nchi 10 zinazoongoza kwa rushwa Duniani.

1. SOMALIA

Nchi hii ya Barani Afrika, ilikuwa bila serikali tangu mwaka 1991. Ndilo taifa linaloongoza kwa ufisadi Afrika na duniani kote. Somalia inaongozwa na Rais wao mpya,Mohamed Abdullahi Mohamed na ina jumla ya watu wapatao milioni 10.79

2. KOREA KASKAZINI

Ikiongozwa na Kim Jong Un, nchi hiyo inapatikana mashariki mwa bara la Asia na ina watu wapatao milioni 25.16

3. MYANMAR

Nchi hiyo awali ilifahamika kama Burma, inapatikana kusini mwa Bara la Asia. Myanmar ni muunganiko wa makundi zaidi ya 100 ya watu wanaotokea katika mipaka ya India, Bangladesh, China, Laos na Thailand. Ina jumla ya watu wapatao milioni 53.9 na inaongozwa na Rais Htin Kyaw

4. AFGHANISTAN

Ni nchi inayoongozwa kwa dini ya Kislam, ipo maeneo ya Kusini katikati mwa bara la Asia, ilawingi wa watu wapatao milioni 32 na inaongozwa na rais Ashraf Ghani.

[caption id="attachment_184173" align="alignnone" width="3912"] An Australian service light armored vehicle drives through Tangi Valley, Afghanistan, March 29. The terrain of Tangi Valley is notoriously rough, but the ASLAV maneuvers across it with ease, said Australian army Lt. McLeod Wood, a troop leader for 2nd Cavalry Regiment, Mentoring Task Force 2, Combined Team Uruzgan.

5. UZBEKISTAN

Lugha inayotumika nchii hii ni kirusi, na inapatikana katikati mwa bara la Asia.

6. TURKMENISTAN

Kwa mujibu wa Banki ya dunia ina watu wapatao milioni 5.374. Rais wao akiwa ni Gurbanguly Berdimuhamedow.

7. SUDAN

Nchi hii inayopatikana kaskazini Barani Afrika inaongozwa na Omar al-Bashir. Lugha ikiwa ni kiarabu na kiingereza. Ina watu wapatao milioni 40.23

8. IRAQ

Ipo Magharibi mwa Bara la Asia, ina watu milioni 36.42 , mji mkuu ukiwa ni Baghdad.

9. HAITI

Inapatikana katika kisiwa cha Hispaniola na ina watu milioni 10.71

10. VENEZUELA

Inapatikana Kusini mwa Amerika na inaongozwa na Rais Nicolás Maduro, ikiwa na jumla ya watu wapatao 31.11

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents