Burudani

Nicki Minaj apotea kwenye mitandao ya kijamii ghafla, yadaiwa uhusiano na Meek Mill umeanza kumharibia

Nicki Minaj amewatia hofu mashabiki wake baada ya kupotea kwenye Instagram na Twitter kwa zaidi ya wiki moja sasa.

nn

Chanzo kilicho karibu na Nicki Minaj kimeuambia mtandao wa Urban Islandz Jumatatu hii kuwa Nicki amepumzika na mitandao ya kijamii ili kurekodi muziki mpya na kutumia muda wake mwenyewe zaidi.

“After constantly being on the road and always working sometimes you need to take some time off to work on your personal life,” kilisema chanzo hicho.

Kiliendelea kuwa Minaj amekuwa kimya kwenye mitandao ili kutumia muda na familia yake. Hata hivyo mashabiki wengine wanahisi kuwa Nicki Minaj anajaribu kuwakwepa mashabiki wanaoupinga uhusiano wake na Meek Mill.

Mashabiki walitumia mitandao ya kijamii kuuponda uhusiano wake na Meek baada ya rapper huyo kuanzisha bifu na Wale. Kitendo cha Meek kudai kuwa Drake huandikiwwa nyimbo zake ziliwafanya mashabiki wa Nicki na Drake walio chini ya lebo moja na kumweka Meek kwenye kitimoto zaidi.

Wakati ambapo Meek Mill anaendelea kutengeneza maadui zaidi, mashabiki wa Nicki wana wasiwasi kuwa vitendo vya Meek vinaanza kuharibu sifa za Minaj.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents