Burudani
Nicki Minaj na Meek Mill kufanya ziara ya pamoja kama ‘Hottest Rap Couple’
Couple mpya inayovuma sana kwa sasa Nicki Minaj na Meek Mill wanaonekana kufata nyayo za Jay Z na Beyonce, wadaiwa kuwa na mipango ya kufanya ziara ya pamoja kama ‘Hottest Rap Couple’.
Vyanzo vya karibu na Nicki na Meek vimeuambia mtandao wa TMZ kuwa couple hiyo inafanya mazungumzo ya kufanya world tour pamoja.
Kwa kuanza, siku ya wapendanao Feb 14. Nicki Minaj na Meek Mill Watatumbuiza kwenye NBA All-Star Weekend huko New York City, itakayofatiwa na show nyingine huko Charlotte mwezi huu.
Taarifa hiyo inaongeza kuwa kutokana na ukubwa wa Nicki, atakuwa analipwa karibia mara mbili zaidi ya Meek .