Nimeshinda mataji 25 na nusu – Mourinho ajiongeza taji lisilomhusu

Kocha machachari na mwenye maneno mengi kunako mchezo wa soka, Jose Mourinho ameamua kujiongezea taji mwenyewe wakati alipotaja idadi ya makombe aliyowahi kushinda kwenye tasnia yake ya mpira.

“Unaweza kuniuliza nimeshinda mataji mangapi katika tasnia yangu ya kocha, nimeshinda 25 na nusu,” – amesema Mourinho ambaye kwa sasa ni kocha mpya wa Roma.

Alipoulizwa na mwandishi wa The Sun ni lipi hilo taji nusu Mourinho amesema “Hilo nusu ni fainali ambayo sikuweza cheza nikiwa na Tottenham.”

Jose Mourinho ameamua kujizawadia nusu ya taji kwa maana sio taji kamili kwa sababu hakuisimamia Tottenham baada ya kuifikisha kwenye mchezo wa finali Carabao Cup.… 🏆✂️

Mourinho amesginda jumla ya mataji 25 ya Ligi ambapo ameyatwaa akiwa Porto, Chelsea, Inter Milan, Real Madrid na Manchester United na alikuwa na nafasi ya kuongeza la 26 akiwa na Tottenham baada ya kuifikisha timu hiyo fainali ya Carabao Cup dhidi ya Man City mwezi Aprili.

Je kwa hisabu zake ana stahili kujipatia nusu wakuwa na mchango wa kuifikisha Tottenham fainali ya Carabao Cup ?

Related Articles

Back to top button