Habari

Ningekuwa na uwezo ningewapeleka Watanzania Ulaya – Mwl Richard Mabala

Muandishi mkongwe wa vitabu nchini Tanzania, Mwalimu Richard Mabala amesema Watanzania wengi hususani vijana wanadhani maisha ya Ulaya ni mazuri lakini kumbe sio hivyo kama wanavyodhani.

Richard Mabala

Mabala akitolea mfano kwa nchi za Marekani na Uingereza amesema Uingereza peke yake kuna watu zaidi ya milioni 3 hawana ajira, wanaishi maisha magumu tena kuna maeneo hata huduma ya maji na umeme hakuna.

Ningekuwa na uwezo ningepeleka watu (Watanzania) wote Ulaya wangegundua kuwa maisha sio kama wanavyofikiria hebu fikiria Uingereza kuna watu milioni 3 hawana kazi kabisa…Wanaishi katika maeneo ambayo umeme ni shida wengine maji hayafanyi kazi na kadhalika kwa hiyo sio kweli kuwa ile ni nchi ya asali na maziwa,“amesema Mwalimu Mabala huku akiendelea kufafanua

Angalia maisha ambayo watu weusi huko Marekani ndiyo maana ikaanzishwa Black Lives Matter kuna matabaka, sasa watu wa hapa wanaangalia tabaka la juu wanafikiri watu wote wanaishi tabaka la juu kumbe wale wanawanyonya watu wa chini ili hao wawe juu,“amesema Mwl. Richard Mabala kwenye mahojiano yake na Times FM.

Mwalimu Richard Mabala ni muandishi mkongwe ambaye amejizolea umaarufu kupitia vitabu vya Hawa The Bus Driver na Mabala The Farmer ni Mtanzania mwenye asili ya Uingereza na aliomba uraia wa Tanzania miaka ya 1970’s.

Katika kufundisha kwake alifanikiwa kuwafundisha Viongozi wengi wakubwa wa taifa letu akiwemo Mh. Dkt. Harisson Mwakyembe ambaye ni Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo na Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi .

By Godfrey Mgallah

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents