Burudani

Nisher ashangazwa na kuvunjwa moyo kwa jinsi ambavyo ‘hakubaliki’ mkoani kwake Arusha!

Jina la ‘Nisher’ limetokea kutajwa sana mwaka huu (2013) kwasababu inaonekana huu ndio mwaka wa kukwea ngazi za kuelekea mafanikio kwa producer na muongozaji wa video Nisher wa Nisher Entertainment ya Arusha.

Nisher

Pamoja na mafanikio ambayo ameanza kuyaona kwa muda mfupi (ikiwa ni pamoja na Jikubali ya Ben Pol kuonekana Ch O) ni ukweli uliowazi kuwa huwezi kumridhisha kila mmoja katika kitu unachokifanya, lakini mara nyingi huwa inaaminika kuwa nyumbani ndio sehemu pekee mtu unaweza kupewa support ya bila kikwazo kitu ambacho kimekuwa tofauti kwa Nisher.

Kupitia ukurasa wake wa facebook Nisher ameelezea hisia zake za masikitiko baada ya kugundua kuwa hakubaliki sana kiwanja chake cha nyumbani (Arusha) na badala yake amekuwa akikubalika zaidi mikoani, kitu ambacho kimemfurahisha kupokelewa vizuri mikoani lakini upande mwingine ameumia kuchukuliwa poa nyumbani alipopategemea angekubalika zaidi kabla ya mikoani.

Hii ndio status ya Nisher:

“Kunakitu naomba niulize….. Mi ni NISHER, sawa but nashangaa Napata upendo mwingisana kwenye Media nyingi sana nchi nzima, Dar, zanzibar, morogoro, iringa mwanza yani hakuna siku sipigiwi simu presenters wanataka interviews na mimi … ila na shangaa A.T.L ambako ndo kwangu watu wachache sana ndo wanajivunia NISHER, this is SO UNBELIEVEBLE NA INANI-VUNJA-MOYO kwamba nyumbani nlitakiwa kupata Love nyingi zaidi KWASABABU NAWAKILISHA MJIWANGU……but inavyoonekana wanao nihitaji na kunionyesha upendo wakweli ni walioko mikoani….. leo nikisema nihamie Huko, Mtaanza ……. Tulijua tu atahama…. mnasahau kua Mi ni MTOTO wenu! Haaaaaya! Mi nawaangalia tu…. Wanao-isifia Mvua, itawanyeshea!! Wasio ihitaji kuna baridi na jua…… –nisher”.

Video ya Ben Pol ‘Jikubali’ imeanza kuonekana Channel O ya Afrika Kusini hivi karibuni, na kwa habari za kitaa inasemekana Video ya Feza Kessy “Amani ya Moyo” pia imepitishwa na kituo hicho (sijathibitisha kwa macho) zote zikiwa zimetayarishwa na kuongozwa na Nisher.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents