Afya

Njia ya kuepuka kutokwa na machozi umenyapo kitunguu

Kuna kitendawili kisemacho nampiga mwanangu nalia mwenyewe, jibu lake ni Kitunguu, kitendawili hiki kimetokana na tabia ya kiungo hicho ambacho hutumika sana wakati wa mapishi, mkataji huwa anatokwa na machozi mara tu anapokata kiungo hicho.

Wengi huamini kuwa machozi hayo hutokana na majimaji yaliyopo kwenye kitunguu bila ya kufahamu nini hasa husababisha macho kuwasha na kutokwa na machozi tofauti na ilivyo kwenye viungo vingine kama Nyanya, Biringanya, Hoho, karoti nk.

Kwa mujibu wa wanasayansi wanaeleza kwamba machozi hutoka wakati wa kukata kitunguu kwa sababu ya kemikali inayoitwa Syn-propanethial-S-Oxide ambayo husisimua tezi ya macho iitwayo Lachrymal ambayo kazi yake ni kuzalisha machozi.

Inaelezwa kuwa wakati unapokata kitunguu, kisu kinavunja seli za kitunguu na kusababisha kemikali hiyo kutoka nje, hivyo basi inapokutana na majimaji ya jicho hubadilika na kuwa acid ya sulphuric ambayo huathiri neva zilizo karibu na machona mwili unaona kama kitisho hivyo hutoa machozi ili kujaribu kusafisha kemikali hiyo na kumlinda mtu kutokana na madhara zaidi.

Hivyo kuvaa miwani wakati wa kukata kitunguu au kuweka kitunguu kwenye maji baridi kabla ya kukata kunaweza kupunguza athari ya kutokwa na machozi.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents