Burudani

One Africa: Enos Olik wa Kenya aongoza video ya Butera Knowles wa Rwanda aliyemshirikisha Roberto wa Zambia

Kiwanda cha muziki cha Afrika kinazidi kuungana pamoja.

12145346_998184826935184_1820880905_n
Kuanzia Kushoto: Butera Knowles, Enos Olik na Roberto

Miaka ya hivi karibuni wasanii wa Afrika wamekuwa wakishirikiana kwenye nyimbo zao za hivyo kuzidi kuusogeza karibu zaidi muziki wa bara hili.

Baada ya kutoka kuongoza video ya wimbo wa Christian Bella na Alikiba ‘Nagharamia’ iliyofanyika nchini Afrika Kusini, Enos Olik ameongoza tena video ya collabo ya wasanii wa Afrika.

1941275_1656963451187936_1818602726_n
Butera na Roberto walipokuwa wakielekea Nairobi kushoot video ya wimbo wao Te Amo

Ni wimbo wa msanii wa Rwanda, Butera Knowles aliomshirikisha hitmaker wa ‘Amarula’ Roberto wa Zambia. Knowles ni msanii mkubwa wa Rwanda kama alivyo Vanessa Mdee kwa Tanzania.

10576237_450318925159477_668963676_n

Video hiyo inafanyika nchini Kenya.

“It’s all smiles with @buteraknowless and @robertozambia. When different cultures meet… #comingsoon,” aliandika Olik kwenye picha aliyoiweka Instagram.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents