Burudani

Oprah awatetea The Kardashians, asema watu wasidharau wanachokifanya wakidhani ni rahisi

Kwa macho ya watu wengi, The Kardashians ni watu waliopata umaarufu na utajiri kwa njia za mkato.

1447091589_oprah-lg

Oprah Winfrey ana mtazamo tofauti. Mtangazaji huyo maarufu wa TV na mwanamke mweusi tajiri zaidi duniani, amedai kuwa The Kardashians ni watu wanaofanya kazi kwa bidii na kujituma kuliko kawaida.

khloe-kourtney-kim-kris-kylie-lg

Akiongea kwenye kipindi cha Kyle and Jackie O Show cha KIIS FM nchini Australia, Jumatatu hii, Oprah alisema aliitembelea familia hiyo na kushangazwa na nidhamu yao ya kazi.

“Niliwahoji miaka miwili iliyopita na siwezi kuamini jinsi wanavyofanya kazi kwa biidii. Watu hawaelewi hilo, watu wanadhani, ‘Oh, Kama kamera za televisheni zinakufuata basi ni rahisi,” alisema Winfrey, 61, kwenye mahojiano hayo.

“Kutengeneza series za reality zinazoonekana kama kitu kinachotokea kweli, kunamaanisha kuwa lazima uwe tayari muda wote.”

“Nilienda kuwahoji kama familia na sikuamini jinsi wanavyojituma. Tulikuwa pale kwa saa saba na walikuwa warekodi kwa masaa mengine saba baada ya mimi kuondoka. Haijalishi wewe ni nani, hiyo ni kazi.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents