Habari

Oprah Winfrey na Barack Obama kutazama mchezo wa fainali ya Kombe la Dunia nchini Kenya

Rais Mstaafu wa Marekani, Barack Obama mwezi ujao anatarajiwa kuzuru nchini Kenya ambapo imeelezwa  kuwa atatembelea hadi kijijini kwa baba yake mzazi.

Barack Obama katikati na Oprah kulia kwenye picha

Kwa mujibu wa taarifa kutoka mtandao wa The Star Obama ataongozana na muandaaji nguli wa vipindi vya runiga duniani, Winfrey Oprah na tajiri namba moja barani Afrika, Aliko Dangote.

Obama na wenzie wanatarajia kuwasili nchini Kenya Julai 15 na kuondoka Julai 16 kuelekea nchini Afrika Kusini ambako atahutubia kwenye mkutano wa 16 wa taasisi ya Nelson Mandela.

Imeelezwa kuwa Obama atakapokuwa nchini Kenya atamtembelea bibi yake katika kijiji cha K’ogelo na baadaye kukutana na Rais Uhuru Kenyatta  na Kiongozi wa Upinzani, Raila Odinga kwa mazungumzo mafupi.

Obama na wenzie watakuwa nchini Kenya katika siku ambayo mchezo wa fainali ya Kombe la dunia utapigwa yaani usiku wa Julai 15, 2018.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents