Michezo

Paul Pogba almasi inayotembea, kumbakiza United kunahitaji mamilioni ya fedha

Mpira umekuwa biashara kubwa kwa sasa duniani huku klabu mbalimbali zikizidi kuwekeza kwenye mchezo huo kwa kutumia mamilioni ya fedha katika kufanya usajili.

Baada ya kumaliza msimu wa 2017/18 ligi kuu Uingereza bila mahusiano mazuri na meneja wake, Pogba amegeuka almasi kwenye dirisha hili la usajili kwa klabu kubwa za Juventus na Barcelona kuhitaji saini yake hii ni kutokana na kiwango kikubwa alichokionyesha kwenye michuano ya kombe la dunia nchini Urusi mwaka 2018.

Katika kuhakikisha usajili wa kijana huyo unakamilika wakala wake ambaye ni Mino Raiola alitua Uingereza siku ya Jumatatu kufanya mazungumzo na Manchester United ya kumuachia kiungo huyo wa Ufaransa kujiunga na miamba ya soka ya Hispania FC Barcelona.

Wakati zoezi hilo likiendelea imeripotiwa kuwa Barca ipo tayari kumlipa Paul Poga pauni 350,000 kwa wiki ikiwa ni sehemu ya usajili wake.

Hatahivyo Man United imegoma kumuachia Pogba na kuitaarifu Barcelona kuwa kamwe haiwezi kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 huku dirisha la usajili likitarajiwa kufungwa kesho siku ya alhamisi na kiungo huyo akihitaji kulipwa pauni 200,000 kwa waajiri wake kama wanahitaji kweli kumbakiza dau ambalo litamfanya kumkaribia  Alexis Sanchez ambaye anaongoza kwa kulipwa mshahara Old Trafford.

Mwezi Agosti mwaka 2016 klabu ya Manchester Unitedilimsajili Paul Pogba kwadau la pauni milioni 89 iliyoweka rekodi ya dunia akitokea Juventus.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents