Michezo

“Phil Jones ndio chanzo cha Hary Kane kuumia, alimkaba sana, Msimu uliopita alikosa michezo 10 kwa jeraha kama hilo” – Pochettino

Meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino amesema ana wasiwasi kwamba Harry Kane aliumia wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England dhidi ya Manchester United – na kwamba huenda ikawaathiri sana.

Kwa mujibu wa BBC, Kane alilalizimika kusaidiwa kuondoka uwanjani Wembley baada ya kuumia dakika za mwisho mwisho kwenye mechi hiyo ambayo United walishinda 1-0.

“Ilikuwa wazi kwamba Harry Kane alichezewa visivyo, aligongwa sana, [mwamuzi] Mike Dean anasema hakuliona tukio hilo,” Pochettino alisema baada ya mechi.”Alikabwa vibaya sana, na sasa kifundo chake cha mguu kimevimba.”

Kane – aliyetoa makombora saba ya kulenga goli ingawa Spurs walishindwa kumbwaga kipa wa United David de Gea – alikuwa ameumia tena kifundo cha mguu mwaka 2018 na alikosa mechi 10 msimu uliotangulia kutokana na jeraha sawa na hilo kwenye kifundo hicho hicho cha mguu.

Kiungo wa kati wa Spurs Moussa Sissoko pia aliumia, na akaondolewa uwanjani kabla ya muda wa mapumziko.

“Haikuwa nia ya mchezaji huyo wa United lakini alimkaba vibaya na Kane alikuwa anachechemea baada ya mechi,” Pochettino aliongeza.

“Tutakuwa pia bila Son Heung-min atakayekwenda kucheza Kombe la Bara Asia na iwapo Kane ataumia, litatwathiri sana. Alipinda kifundo chake cha mguu na tunatumai kwamba halitakuwa jeraha mbaya sana.”

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents