Burudani

Picha: Ben Pol ashare picha ya mwanae kwenye mtandao

Msanii wa muziki wa R&B, Benard Paul ‘Ben Pol’, ameamua kushare picha ya mwanae aitwae ‘Mali’ katika mitandao ya kijamii.
13509106_1294459490584992_6976919684938829733_n
Mtoto wa Ben Pol aitwae ‘Mali’

Muimbaji huyo wa wimbo ‘Moyo Mashine’ unaofanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio na runinga, kupitia instagram yake, ameandika ujumbe wa mwanae kwa mashabiki wake.

“Shikamooni watu wa Baba yangu’ wa Instagram na Facebook… Nimewamiss… faza kaniambia nije niwasalimie kidogo, jina langu mi apa aitwa Mali ya Baba , I’m out! Oyo aasshinee, imba na Baba ????” twende wote ???????? Byee,” aliandika Ben Pol katika picha hiyo hapo juu.

Muimbaji huyo alikaririwa na vyombo vya habari akisema kwamba albamu yake mpya inayokuja itaitwa ‘Mali’ jina la mwanae huyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents