Burudani

Picha: Dj Tass apata shavu la kuhost TV show ya ‘Wakilisha’ kupitia channel mpya ‘Maisha Magic’ ya DSTV

Wiki iliyopita M-Net imezindua channel mpya iitwayo ‘Maisha Magic’, itakayokuwa ikionesha maudhui ya Afrika Mashariki kupitia channel 161 ya DSTV. Dj Tass wa Magic Fm ya Tanzania amepata shavu la kuwa host wa show iitwayo ‘Wakilisha’ itakayokuwa ikirushwa kwenye channel hiyo mpya.

m-net maisha magic

Dj Tass ambaye weekend iliyopita alienda Nairobi kurekodi show hiyo, ameiambia Bongo5 kuwa amepata shavu la kuwa Dj na mtangazaji wa show hiyo mpya itakayokuwa ikipromote muziki wa Afrika mashariki.

IMG-20140907-WA0007
Dj Tass akiwa Nairobi

“Wakilisha ni kipindi kipya ambacho kinaruka kupitia channel mpya ya Maisha Magic ya DSTV channel 161, ambacho kinapromoti muziki wa Afrika mashariki tu, Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, na Burundi.”

IMG-20140907-WA0006
Dj Tass wakati akirekodi kipindi cha ‘Wakilisha’ Nairobi

Aliongeza,

“Yah kimeanza 1/9/2014 na kinaendeshwa na mimi Dj Tass, kitakuwa kikiruka kila Jumatatu hadi Ijumaa saa kumi jioni na kurudiwa saa mbili asubuhi, hivyo hii ni fursa nzuri kwa wasanii wa Afrika mashariki.”

Kuhusu kama kutokana na shavu hilo jipya amehama moja kwa moja Magic Fm na kuhamia Kenya ambako ndiko wanakorekodia kipindi hicho, Tass alisema,

“Sijahama Magic Fm bado nakamua ‘Daladala beats na Kwetu Fleva kama kawaida”.

IMG-20140908-WA0002

IMG-20140908-WA0003

IMG-20140908-WA0004

IMG-20140908-WA0005

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents