Burudani

Picha: Jacqueline Mengi azindua duka la furniture za nyumbani ‘Amorette’

Miss Tanzania 2000, Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi, Alhamisi hii amezindua duka lake jipya ‘Amorette’ lililopo Sea Cliff Masaki jijini Dar es salaam ambalo litakuwa likiuza furniture za ndani za brand yake ya ‘Molocaho’.

img_9737
Jacqueline Mengi akiongea na waandishi wa habari

Duka hilo linauza vitu vya aina tofauti tofauti kama makochi, viti, vitanda, meza na baadhi ya vitu vingine huku akitarajia kuongeza kwa kuuza furniture za jikoni kwa hapo baadae.

Akiongea katika uzinduzi huo Alhamisi hii, Jacqueline Mengi amesema kuwa mahitaji makubwa ya furniture za majumbani ni kitu ambacho kimemsukuma kufanya biashara hiyo.

“Amorette ni kampuni ambayo nilianzisha miaka michache iliyopita, tunafanya interior designing. Kwahiyo ndio nikaanzisha brand inaitwa Molocaho, na bidhaa zote ambazo zinazalishwa hapa zitakuwa na nembo ya Molocaho,” alisema Jacqueline.

Aliongeza, “Nilianza kudisign furniture kwa sababu niliona kuna ukosefu wa furniture ambazo ni unique, kwahiyo nikaona kwamba hii ni nafasi nzuri ya mimi kutengeneza furniture ambazo zitakuwa ni tofauti na ambazo zinapatikana kwenye market, lakini pia kutengeneza vitu ambavyo vipo kwenye viwango vya kimataifa. Mimi kama designer kwangu najisikia furaha kutumia muda wangu kudisign vitu.”

img_9692
Jacqueline Mengi akiwa na Balozi Juma Mwapachu pamoja na wageni wengine waalikwa

img_9813-copy
Jacqueline Mengi akiwa na rafiki zake

img_1208

img_1204-copy

img_1182

img_9758

img_1190-copy

img_1165-copy

img_1185-copy

img_1187-copy

img_1184

img_1183

img_1211

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents