Habari

Picha: Matukio yaliyojiri Bungeni Dodoma

Jumatano hii, katika kikao cha 60, mkutano wa 7 Bunge la 11 mjini Dodoma, leo ilikuwa ni siku ya kuahirishwa kwa Mkutano wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuendelea hadi tarehe 5, Septemba mwaka huu siku ya Jumanne.


Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dk.Tulia Ackson akiongoza kikao cha sitini cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo


Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe.George Masaju akisoma maelezo ya Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali wa mwaka 2017 katika kikao sitini cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo

PICHA ZOTE NA MAELEZO,DODOMA

Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Mhe.Eng Stella Manyanya akijibu maswali mbalimbali ya wabunge kikao cha sitini cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo


Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.Dk Ashatu Kijaji akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha sitini cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo


Viongozi na wachezaji wa timu ya Singida United wakiwa wakifuatilia mijadala ya bunge katika kikao cha sitini cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo

Bunge limehairishwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents