Michezo

Picha: Messi alivyokutana na mtoto aliyevaa mfuko wa plastiki wenye jina lake

Mtoto wa kiume mwenye uraia wa taifa la Afghanistan ambaye alikuwa gumzo katika mitandao ya kijamii kwa ku vaa fulana ya mfuko wa plastiki ilio na jina la Lionel Messi hatimaye amefanikiwa kukutana na shujaa wake huyo kutoka Argentina.


Messi na Murtaza Ahmadi mjini Doha

Picha ya Murtaza Ahmadi, mwenye miaka sita, akiwa amevalia karatasi hiyo iliyoandika nambari ya jezi ya Messi pamoja na jina lake ilivuma sana mwezi Januari mtandaoni.


Murtaza akiwa amevalia jezi yake ya karatasi, iliyovuma sana mtandaoni

Mwishowe, alipokea jezi halisi kutoka kwa mshambuliaji huyo wa Barcelona, ambayo pia ilikuwa imetiwa saini na mchezjai huyo.


Murtaza akiwa na jezi aliyotumiwa na Messi

Lionel Messi amafanikiwa kukutana na Murtaza Ahmadi mjini Doha, kwa mujibu wa kamati andalizi ya Kombe la Dunia la 2022 nchini Qatar.

Barcelona wamo nchini Qatar kucheza mechi ya kirafiki na Al Ahli Jumanne.

Ahmadi anatarajiwa kutembea kuingia uwanjani akiandamana na Messi.

“Ni picha ambayo ulimwengu ulitaka kuona,” aliandika mkuu wa kamati hiyo Jumanne.

“Mvulana wa miaka sita akikutana na shujaa wake, #Messi, ndoto yake ikitimia.”

Ahmadi, ambaye anatoka wilaya ya Jaghori, katika mkoa wa Ghazni mashariki mwa Afghanistan, alilazimika kukimbilia nchi jirani ya Pakistan mwezi Mei.

Murtaza ambaye picha yake ilisambazwa mtandaoni na mjomba wake ambaye ni Azim Ahmadi, raia wa Afghanistan anayeishi Australia, nabaadae aliwaunganisha waandishi wa BBC Trending na nduguye, Arif – babake ambaye ni shabiki mkubwa wa Messi.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents