Burudani

Rick Ross adai Kanye West alijifanya kuumwa ili kupata kiki

Wakati Kanye West akipambana kurudi kwenye hali yake ya kawaida kutokana na kusumbuliwa na matatizo ya akili, Rick Ross ameibuka na kudai anaamini kuwa rapper huyo haumwi ila ameamua kuidanganya dunia.

Akiwa kwenye onesho mjini New York Jumatatu hii, rapper huyo amesema, “One time for Yeezy … My homie a genius. For everybody who thought he was wigging out, he played y’all niggas.”

Mwezi uliopita West alilazwa kwenye hospitali ya UCLA Medical Center ya mjini Los Angeles kwa siku 10 na kusitisha ziara yake ya Saint Pablo. Kwa sasa rapper huyo anaishi kwenye jumba lake la kifahari la Bel-Air chini ya uangalizi wa daktari maalum.

Hata hivyo, Jumatatu hii rapper huyo ameonekana akikatiza mitaa ya New York.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents