Burudani

Picha: Mfahamu mpenzi mpya wa Rihanna

Je unamfahamu mpenzi mpya wa Rihanna? Wiki iliyopita muimbaji huyo aliwashtua mashabiki kutokana na picha zake zikimuonyesha akiwa anakula bata nchini Hispania na njemba ambaye hakuweza kufahamika kwa mara moja.


Moja ya picha ya Rihanna na Jameel ikiwaonyesha wakila raha nchini Hispania wiki iliyopita

Baada ya upelelezi wa kina jina la kidume huyo likafahamika kuwa ni Hassan Jameel ambaye ni raia wa Saudi Arabia.


Hassan Jameel akihutubia kwenye moja ya mkutano wa kibiashara nchini Saudi Arabia

Jameel anadaiwa kutoka kwenye familia ya kitajiri huku yeye mwenyewe akitajwa kumiliki utajiri wa kiasi cha dola bilioni 1.5. Tajiri huyo pia ana haki miliki ya uuzaji magari aina ya Toyota nchini Saudi Arabia pamoja na kumiliki ligi ya mpira wa miguu ya nchini humo iitwayo Jameel League.

Wakati huo huo Jameel mwenye miaka 29 anatajwa kuwahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanamitindo na muigizaji maarufu Naomi Campbell.


Picha ya Naomi Campbell akiwa na ex wake Jameel waliyopigwa mwezi Julai mwaka 2016

Hata hivyo Naomi hajaonyesha kuumizwa zaidi na mahusiano hayo mapya ya Rihanna na Hassan.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents