Burudani

Picha: Wastara onesha miguu yake kwa mara ya kwanza toka alipokatwa mguu mmoja miaka 6 iliyopita

Weekend iliyopita muigizaji mrembo wa filamu za Bongo, Wastara Juma aliamua kuweka wazi kile kinachoendelea kwenye maisha yake toka alipokatwa mguu wake wa kulia miaka 6 iliyopita.

Wastara

Akiwa jijini Nairobi kwenye matibabu, Wastara alipost picha hii kwenye akaunti yake ya Intagram na kuandika ujumbe ufuatao;

wastara mguu

“Kwa mara ya kwanza toka nimekatwa mguu miaka 6 iliyopita leo nimechukua nafasi hii kupost hii pic kuondoa maswali mengi yaliyopo vichwani mwa watu
Nipo kma unavyoiona pic.

Huyo ndio wastara nilivyo hakuna kilichopungua zaidi ya hicho unachokiona
Kuwa mlemavu ni kitu kingine tofauti ukiwa mzima hivyo kusikia maumivu na kuumwa mguu ni kitu cha kawaida.

Sasa nipo nairobi kimatibabu na tatizo ni operetion ya kwanza nilikosewa ndio sababu ya maumivu ya mara kwa mara madaktari wameshajua nini cha kunifanya ili kuondoa mateso kwangu .

Jifunze kitu kupitia hii pic yangu na si kucoment ujinga jiulize ungekuwa wew mama yako dada yako mume,mke, wako ungeweza kusmile kma mimi hali ya kuwa una maumivu?

Jifunze kitu kupitia wastara na sijajidharirisha nimetaka wew unijue nilivyo ili usiteseke na maswali juu yangu.
Sijakatwa miguu yote kma ilivyovumishwa na pia pamoja na maumivu ninaweza kutembea japo si mwendo mrefu sana na naendelea kusmile.
SOTE TUSEME ALHMADULILAH
ASANTE MUNGU”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents