Burudani

Picha: Yamoto Band wawasili Afrika Kusini tayari kushoot video ya ‘Cheza Kimadoido’ na Godfather

Ndoto za vijana waliotegenezwa na Mkubwa Fella, Yamoto Band za kwenda kimataifa zinaelekea kutimia. Vijana hao wamewasili jana nchini Afrika Kusini, ambako wameenda kushoot video yao ya kwanza kuwahi kufanya na director mkubwa wa nje.

yamoto na Godfather
Yamoto na uongozi wao wakifanya kikao na Godfather

Yamoto wameshare picha wakiwa Afrika Kusini na uongozi wao, Said Fella, Babu Tale na Diamond. Katika picha hizo walionekana wakiwa kwenye kikao na director atakayefanya video yao Godfather.

yamoto na Godfather-2

“Hii ni mipango ya video jinsi itavyokuwa yani jinsi gan itaanza na itaisha asante mungu asante pia@mkubwafella @babutale @diamondplatnumz@i_am_godfather dua zenu 2 wadau amen.” aliandika muimbaji wa band hiyo Beka kwenye moja ya picha hizo.

“Mikakati inaanza na @i_am_godfather na vijanaa wa @yamoto_band kuhusu video kesho na kaka yao @diamondplatnumz mungu tushikie wajawako na hili” Aliandika Babu Tale

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents