Michezo

Pitso Mosimane majanga yamkuta

Kocha Pitso Mosimane raia wa Afrika Kusini amekuwa na wakati mgumu tangu ajiunge na klabu ya Abha FC ya nchini Saudi Arabia inayoshiriki Ligi ya Saudi Pro League, Kocha huyo amekuwa na upepo mbaya wa vipigo tangu ajiunge na klabu hiyo ambapo jana amepoteza tena kwa kufungwa magoli 5-0 dhidi ya Al Shabaab.

Msimu hue Pitso ameiongeza klabu hiyo kwenye jumla ya michezo 23 kwenye mashindano yote aliyoshiriki huku akishinda michezo 11 sare 3 na kupoteza michezo 9 na kwenye Ligi ya Saudi Pro League anashika nafasi ya 15 ambayo ni ya 4 kutoka mwisho.

Kwenye michezo 5 ya mwisho Pitso amepoteza michezo 3 sare 1 na kushinda 1 huku akipokea kipigo cha magoli 8-0 dhidi ya Al Nassr na akipoteza tena jana kwa Mabao 5-0 dhidi ya Al Shabaab.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents