Michezo

Kobbie Mainoo ndio basi tena

Manchester United imepanga kumpa ofa ya dili safi kabisa kiungo Kobbie Mainoo huku bilionea mpya wa miamba hiyo ya Old Trafford, Sir Jim Ratcliffe akitaka kujenga kikosi kipya kutokana na kinda huyo.

Mainoo 18, amekuwa mchezaji muhimu sana kwenye kikosi cha Man United kwa sasa chini ya Kocha Erik ten Hag.

Man Utd inataka kumwongezea mshahara Mainoo kwa sababu inamhesabu kama mmoja wa wachezaji ambao wapo kwenye mipango mipya ya bilionea Ractliffe katika kuifumua na kuitengeneza upya timu hiyo ili kuwa tishio Uwanjani.

Fabrizio Romano alisema “Ipo hivi Man Utd kwa sasa ipo kwenye mazungumzo ya kumuongezea mkataba Kobbie Mainoo itakapofikia mwisho wa msimu na mjadala huo ulianza Februari.

INEOS inamtaka Kobbie awe mmoja wa mastaa watakaokuwa kwenye mpango mpya wa timu hiyo. Dili jipya litashuhudia mshahara wa Maino ukiongezeka pamoja na Bonasi kadhaa. “Kiungo huyo anaripotiwa kulipwa Pauni 20,000 kwa Wiki na sasa kuna kila dalili mshahara wake ukaongezeka mara tatu atakaposaini dili jipya ili kubaki Old Trafford.

Mainoo amecheza mechi 27 kwenye kikosi cha Man United kwenye michuano yote msimu huu na amefunga mabao matatu na asisti mbili. Amejumuishwa pia kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya England wakati kikosi hicho cha Kocha Gareth Southgate kulipocheza na Brazil na Ubelgiji kwenye mechi za kirafiki.

Mainoo amekuwa kwenye kikosi cha Man United tangu alipokuwa na Umri wa miaka tisa. Makinda wengine wanaotazamiwa kuwapo kwenye mpango mpya wa Man United ni Alejandro Garnacho na beki wa kati Willy Kambwala.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents