Burudani

Pole Jay Z: Sony yapanga kuzitoa nyimbo za Beyonce kwenye mtandao wa Tidal

Miezi michache baada ya kuuzindua mtandao wake wa Tidal, Jay Z ameanza kupata pigo.

beyonce-jay-z-working-album

Bloomberg Businessweek imeripoti kuwa label ya Sony inataka kutolewa kwa nyimbo zake zote kwenye mtandao huo, zikiwemo za mke wake Beyonce ambaye pia ni mmiliki mwenza wa mtandao huo.

Kwa mujibu wa vyanzo, Jay Z bado hajakamilisha makubaliano ya mkataba na Sony ambao wanataka walipwe kiasi kikubwa cha fedha kama kianzio kwaajili ya kutoa haki za kuwekwa kwa nyimbo zao.

Universal na Warner tayari wameshamaliza makubaliano na Tidal.

Kama Jay Z atashindwa kuwalipa Sony fedha wanayoitaka, Bloomberg imesema nyimbo za wasanii wake wengine wakiwemo Daft Punk, Alicia Keys, na Usher zitaondolewa kwenye Tidal.

Hivi karibuni Sony ilifuta nyimbo zake kutoka kwenye mtandao wa SoundCloud kwa sababu hizo hizo. Hata hivyo Bloomberg imedai kuwa Tidal iko vizuri kifedha na hivyo hili linaweza kuwa ni suala dogo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents