Michezo

Promota hajanilipa pesa zangu mpaka leo, pambano na Mthailand Sirimongkhon -Twaha Kiduku (+Video)

Bondia Mtanzania Twaha Kiduku ameiyambia Bongo5 kuwa mpaka sasa hajalipwa fedha zake zilizobaki ambazo amedai ni nyingi mno ukilinganisha na kiasi kidogo alicho chukua kama utangulizi katika pambano lake dhidi ya Mthailand Sirimongkhon lililopigwa kwenye ukumbi wa PTA Sabasaba ambapo alishinda kwa TKO usiku huo wa Vitasa.

Twaha Kiduku ameyasema hayo baada ya kuandika ujumbe ambao unawatetea Mabondia wenzake waliyokosa nauli ya kurejea kwao Simbawanga pamoja na hela ya kula wakiwa Dodoma baada ya kukimbiwa na Promota licha ya kuandikishiana mikataba.

”Pambano langu na Mthailand sijalipwa pesa zangu, nilipata robo tu ya pes zote, Promota Shomari Kimbau. Viongozi wa mchezo wa Ngumi wapo kimya tu, sijui wanachoshindwa ni nini ?, naiomba serikali iingize mkono wake, pambano langu sijalipwa hela na wala mpaka leo halijaingizwa kwenye rekodiĀ  ?”

Twaha Kiduku alishinda pambano hilo kwa TKO dhidi ya Mthailand Sirimongkhon raundi ya 7, pambano la uzito wa kati lililopigwa Oktoba 30, 2020 kwenye ukumbi wa PTA Sabasaba.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents