Uncategorized

Pusha T amchokonoa Drake baada ya jina lake kukosekana kwenye tuzo za Grammy

Rapper kutoka Marekani Terrence LeVarr Thornton Pusha T amefunguka mengi kuhusu bifu lake na Drake lakini pia kikubwa zaidi kuhusu Drake kukosekana katika kipengele chochote katika tuzo za Grammy.

Pusha T amefunguka baada ya hasimu wake kukosekana huku yeye akiwepo katika tuzo hizo:-

Pusha T amesema:- ”

“Nafikiri kila mmoja anatakiwa kukaa kwenye kipengele chake anachostahili” alisema Pusha T baada ya kuulizwa juu ya hasimu wake, Drake kukosekana kwenye kipengele cha Rap Album Of The Year kwenye tuzo za Grammy 2019.

King Pusha amemchokoza Drake, kwenye mahojiano na Associated Press alizungumzia bifu yake na The Scorpion rapper huku akisisitiza kuwa kutokuwepo kwenye kipengele hicho kunaleta maana kuwa hawafanani na anachokifanya (Drake) sio Hip Hop.

Hapana, Sikushangazwa na yeye kukosekana kwenye kipengele. Nafikiri kila mmoja anatakiwa kukaa kwenye kipengele chake anachostahili. Sifikirii kwamba mimi na yeye tupo kwenye kipengele kimoja.” alisema Pusha T.

Kuingia kwenye bifu na Drake kipindi ameitoa album yake ‘Daytona’ amesema hakupanga iwe hivyo ila ilivyokuja imempa nyongeza ya promotion ‘extra credit’

Pusha ametajwa kuwania kipengele cha Best Rap Album kwenye Grammy 2019 kupitia album yake ‘Daytona’

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents