HabariSiasa

Rais akataa kujiuzulu kwa Waziri Mkuu Mario Draghi, Itali

Rais wa Italia Sergio Mattarella ametangaza jana usiku kwamba hatokubali hatua ya kujiuzulu kwa waziri mkuu Mario Draghi.

Waziri Mkuu Draghi alisema angejiuzulu baada ya vuguvugu la Nyota Tano kuondoa uungaji wake mkono kwa serikali.

Draghi alinusurika kura ya imani katika bunge la Italia kwa kushinda kura 172-39.

Wabunge wa vuguvugu la Nyota Tano walikataa kushiriki kura hiyo, wakieleza upinzani dhidi ya baadhi ya vipengele vya mpango wa euro bilioni 26 wa kutuliza bei za nishati zinazozidi kupaa.

Draghi alikuwa amesema hana nia ya kuongoza bila vuguvugu la Nyota Tano. Ofisi ya Mattarella imesema hakukubali kujiuzulu, na kumualika Draghi kujitokeza mbele ya bunge.

Mkuu huyo wa zamani wa Benki Kuu ya Ulaya, ECB, alichaguliwa kuwa waziri mkuu wa sita wa Italia katika miaka 10 mwaka 2021.

Endapo Draghi atashindwa kuunda serikali ya muungano, Mattarella huenda akalivunja bunge na kuitisha uchaguzi mpya mwezi Septemba.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents