Habari
Rais Dkt. Samia atengua uteuzi wa Diwani
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Kamishna Diwani Athumani Msuya aliyemteua tarehe 3 Januari, 2023 kuwa Katibu Mkuu Ikulu.
Aidha Rais Samia amemteua Bw. MululiĀ Majula Mahendeka kuwa Katibu Mkuu Ikulu. Bw. Mahendeka alikuwa Afisa Mwandamizi wa Ofisi ya Rais, Ikulu.