Habari

Rais Museveni kuapishwa leo

Rais wa Uganda Yoweri Museveni anatarajiwa kuapishwa Jumatano hii kwa muhula wake wa sita.

Tukio la kuapishwa kwa Raishuyo wa Jamhuri ya Uganda, Yoweri Kaguta Museveni litafanyika katika uwanja wa sherehe wa Kololo Jijini Kampala.

Usalama umeongezwa katika mji Mkuu, Kampala, kabla ya kuapishwa kwake.

Wakuu wa nchi kadhaa tayari wamewasili kwenye sherehe hiyo – pamoja na kutoka Tanzania, Burundi, Sudan Kusini na Somalia.

Siku ya Jumatatu, polisi walisema zaidi ya watu 40 walikamatwa kwa kupanga kuvuruga sherehe hiyo.

Askari wamezunguka nyumba ya Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine, ambaye alikuwa mshindi wa pili wa uchaguzi.

Museveni alishinda uchaguzi mkuu uliyofanyika mwezi Januari 2021.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents