Siasa

Rais Samia awatoa hofu kuhusu ahadi ya kupandisha mishahara

Rais Samia Suluhu Hassan amewahakikishia wafanyakazi kuwa ahadi ya kuwaongezea Mshahara aliyoitoa mwaka jana wakati wa sherehe za Mei Mosi jijini Mwanza ipo pale pale.

Akihutubia wakati wa sherehe za mwaka huu za siku ya wafanyakazi Duniani zinazofanyika Mkoani Dodoma, Rais Samia amesema “lile jambo letu lipo ila sio kama lilivyosemwa na TUCTA” akimaanisha utekelezaji wa ahadi hiyo upo pale pale

”Ninakubaliana nanyi kwamba viwango vya mishahara vya sasa havikidhi mahitaji, ili kuendelea kulinda maslahi ya Wafanyakazi, Serikali imeshaunda Bodi za Kima cha Chini cha Mishahara kwa sekta zote na tayari zimeanza kufanya tathmini ili kufanya maboresho.”- Rais Samia Suluhu Hassan

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents