Siasa

Rais wa Brazil Bolsonaro: Raia acheni kulialia kuhusu Corona, mtalia mpaka lini (+ Video)

Rais Jair Bolsonaro amewataka raia wa Brazil ”waache kulialia” kuhusu Covid-19, akikosoa njia zinazotumika kupambana na virusi pamoja na kuwepo ongezeko la maambukizi na vifo.

Kauli yake imekuja siku moja baada ya Brazil kushuhudia ongezeko la vifo katika kipindi cha saa 24.

Brazili imeathirika vibaya na janga la corona, na kuacha mfumo wa afya ukiwa katika hali mbaya.

Katika kupambana na hali hiyo baadhi ya miji na majimbo yameweka mashati yao wenyewe.

Wizara ya Afya nchini humo imesema zaidi ya watu 260,000 wamekufa kutokana na Covid-19, ikiwa ni nchi ya pili duniani baada ya Marekani.

Pamoja na hali hiyo, Bw. Bolsonaro ameendelea kudhihaki tishio linalosababishwa na virusi hivyo.

”Acheni kulialia, mtalia mpaka lini?” Bolsonaro alisema. ”mtakaa nyumbani mpaka lini na kufunga kila kitu? hakuna atakayeendelea kuvumilia. Tunasikitika kuhusu vifo, lakini tunahitaji ufumbuzi.

Rais Bolsonaro amekuwa akipinga hatua za kukaa karantini zilizowekwa na magavana, akisema kuwa ni hatari kwa uchumi wa taifa hilo kuliko hatari inayosababishwa na virusi vyenyewe.

Bofya hapa kutazama.

https://www.instagram.com/tv/CMElij6hmw4/

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents