Rais Yoweri Museveni atishia kuyaondoa majeshi yake Somalia, aeleza sababu

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametishia kuyaondoa majeshi ya nchi yake katika mpango wa usalama nchini Somalia.

Licha ya kwamba sio mara ya kwanza kwa Rais huyo kutishia ,amekuwa akifanya hivyo baada ya viongozi wa nchi hiyo kuhatarisha amani ya nchi hiyo na mpango wa uchaguzi unaopangwa kufanyika.

Akizungumza na chombo cha habari cha Ufaransa ‘France 24’ Rais Museveni amejibu swali aliloulizwa kuhusu mpango wake wa kuondoa majeshi yake ya UPDF nchini Somalia baada ya ongezeko la mashambulizi kutoka kwenye kundi la waasi la Al-Shabab pamoja na mgogoro wa kisiasa nhini humo.

Akielezea mgogoro wa kisiasa nchini Somalia mwaka 2011, Museveni alitaka maelewano ambayo yalipelekea kujiuzulu kwa aliyekuwa

Waziri Mkuu kipindi hicho Mohamed Abdullahi Farmaajo ambaye kwa sasa anahudumu kama Rais na katika kipindi hicho Museveni alitishia kuondoa majeshi yake.

Uganda inakuwa nchi ya kwanza kupeleka majeshi yake nchini Somalia kupitia mwamvuli wa kulinda amani Afrika wa mwaka 2007.

Wakati huo, Al-Qaeda wakishirikiana na Al-Shabaab walitishia kuiondoa madarakani serikali iliyokuwa ikungwa mkono na mataifa ya Magharibi. Wiki chache baadae, Uganda ilituma jeshi lake baada ya Azimio la Umoja wa Mataifa lililofanyika mwezi Machi, kuusaidia Umoja wa Afrika nchini Somalia hadi Disemba mwaka huu.

Museveni akielezea juu ya msimamo wake alisema kuwa hana imani sana majeshi yanayotoka nje ya Afrika lakini kutokana na kwamba kazi inayopaswa kufanywa ni kubwa basi hakukuwa na muda kushikilia maneno yake.

Amesema kuwa, maamuzi ya kujiondoa kwa majeshi yake yanaweza kufuata utaratibu wa mazungumzo na Umoja wa Afrika lakini ameona ni muda sasa wa wao wajilinde wenyewe.

Siku ya jumatatu, majibizano baina ya Rais na Waziri Mkuu wa Somalia yameendelea baada tu ya kufukuzwa kazi mkuu wa kitengo cha usalama wa taifa.

Hata hivyo, inawezekana uchaguzi uliopangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Oktoba mwaka huu ukasogezwa mbele baada ya uchaguzi wa wabunge kupelekwa mbele mwisho wa mwezi Novemba.

Related Articles

Back to top button