Michezo

Rasmi waliyoshinda mkwanja wa zaidi ya Milioni 825 na kuvunja rekodi wakabidhiwa mbele ya wanahabari 

Dar es salaam, Baada ya Jackpot ya SportPesa kuvunjwa kwa mara ya kwanza ikiwa imefikia jumla ya milioni 825,913,640/= na washindi wawili kupatikana,leo hii wamekabidhiwa rasmi mkwanja wao kila mmoja akichomoka na kitita cha milioni 412,956,820/= baada ya kubashiri kwa usahihi mechi kumi na tatu za Jackpot wiki
iliyopita.

Image

Kingsley Simon Pascal mwenye umri wa miaka 26 akitokea Biharamlo ndiye mshindiwa kwanza wa Jackpot na mshindi mwingine ni Magabe Matiko Marwa mwenyemiaka 31 akitokea wilaya ya Serengeti wote wakigawana kwa usawa kitita hicho cha Jackpot.

Mkurugenzi wa utawala na udhibiti wa SportPesa ndugu Tarimba Abbas akizungumza wakati wa kuwakabidhi hundi kwa washindi hao wa kihistoria alisema,”Nafurahia kuwakabidhi washindi wetu wa shilingi milioni 825,913640/= za Jackpot yetu ambayo ndiyo kubwa zaidi nchini,ni hii ikiwa ni mara ya kwanza kwenye historia ya betting Tanzania kwa kiasi kama hichi kutolewa kwa washinidi wa michezo ya kubahatisha aliendelea kwa kusema “‘’Naomba
mtambua kila wiki watu wanacheza michezo mbali mbali na Sportpesa ila kwenye hii segment ya Jackpot tangu tumeanza tumetoa zaidi ya bilioni 4.4 kwa washindi na kati pesa hizi kodi ni million 864 na hutujawahi kupata
malalamiko kutoka kwa washindi wetu na wamekuwa wakituamini na kuwa na uhakika wa kushinda.’’

Image

Kwa upande wa washindi kila mmoja akionyesha furaha ya kipekee wakifurahia ushindi wao, na wote wakikiri kuwa iliwachukua muda kuamini kama kweli pesa zote hizo ni za kwao, Magabe Matiko Marwa ambaye pia ni mshindi wa Bonus za Jackpot wiki iliyopita akiwa na mke wake Bi Elizabeth Wambura alionekana kuwa na furaha
isiyo ya kawaida kabisa.

“Leo ndio nimeamini rasmi mara baada ya kukabidhiwa fedha hizi na kuamini kwa macho yangu kama nimeshinda, naomba watanzania waamini kuwa mimi nimeshinda kweli na si vinginevyo.”

“Watanzania waamini mimi sifahamiani na mtu yoyote SportPesa na kuibuka mshindi niliweka mkeka mmoja wa shilingi 2000/= tu”

Kingsley alipoulizwa kuhusu watu wasioamini kama wanaweza kushinda alisema,’’huwezi kupata kitu usipojaribu na mimi ni mtu wa kujaribu vitu vingi na sasa ni mshindi wa Jackpot nachoweza kusema kila mtu anaweza kushinda akijiamini na kuweka nia bila kukata tamaa.”

“Tangu nianze kubet Jackpot mwezi wa tatu mwaka huu hii ni mara ya 17 kama si 16 na nimebahatika kuibuka mshindi wa mil 412,956,820/=” Changamkia fursa kwa kucheza Jackpot mpya ya SportPesa dau likiwa milioni 200
kwa kupiga *150*87# au temebelea www.sportpesa.co.tz

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents