HabariSiasa

RC Makalla: Operesheni ya kukamata Panya Road imekuwa na mafanikio makubwa, iendelee

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amesema kwa siku nne tangu kuanza kwa Operesheni ya kukabiliana na Panya Road Mkoa upo salama Baada ya kufanikiwa kuwakamata Watuhumiwa 135 na Vifaa mbalimbali vilivyoibiwa.

RC Makalla amesema hayo wakati wa kikao kazi Cha Kamati ya Ulinzi na usalama kilichoketi kufanya tathimini ya Hali ya usalama Mkoa pamoja na kupokea taarifa ya mwenendo wa Operesheni ya kukamata Wahalifu.

Ili kuhakikisha matukio hayo hayajirudui, RC Makalla amebainisha mipango ya kudhibiti uhalifu ikiwemo Vituo vyote vya polisi kufanya kazi kwa saa 24, Ongezeko la Doria kila Kata, Kila Mtaa kufanya mkutano maalumu kujadili ajenda ya Ulinzi na usalama kila wiki ya kwanza ya Mwezi.

Aidha RC Makalla amesema mipango mingine ni msako kwa Wafanyabiashara wanaouza na kununua Vifaa vya Wizi, Kuimarisha Vikundi vya ulinzi Shirikishi, ufuatiliaji wa mienendo wafungwa waliomaliza kutunikia vifungo na msako kwenye vijiwe, majumba mabovu yasiyokamilika (Mapagala) na vibanda umiza ambavyo vimekuwa sehemu ya kukutana na kuweka mipango.

Pamoja na hayo RC Makalla ametoa wito kwa Wazazi kuhakikisha wanazingatia suala la malezi kwa kufuatilia mienendo ya watoto wao.

Operesheni ya kukamata Panya Road ilizinduliwa September 15 na ndani ya siku nne imekuwa na mafanikio makubwa yaliyopelekea kukamatwa kwa Watuhumiwa 135, Wanunuzi 5 wa Vifaa vya Wizi na kupatikana kwa Mali zilizoibiwa ikiwemo Tv, Radio, simu za mkononi na vitu vingine.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents