Burudani

RC Makonda awaonya Alikiba na Diamond Platnumz

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Mhe Paul Makonda amefurahishwa na ushindani wa kimuziki baina ya Diamond Platnumz na Alikiba kwa kusema unachangamsha muziki wetu huku akiwaonya kuwa kazi zao lazima wazingatie sheria na maadili yetu.

Mhe Paul Makonda

Mhe Makonda amesema anapenda sana anavyowaona vijana hao wakishindana na ushindani wao unafanya muziki ukue kwa kufanya kazi nzuri.

Tofauti zenu mimi nazipenda, kwani zinaleta ushindani mzuri kwenye mziki“,ameandika Mhe Paul Makonda kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuwaonya kuwa ni lazima wazingatie sheria na utamaduni wetu kwenye kazi zao kwa kusema “Ila naomba mzingatie sheria na Utamaduni wetu..“.

SOMA ZAIDI- Video ya ‘Seduce Me’ ya Alikiba yavunja rekodi ya ‘Salome’ ya Diamond Platnumz

Alikiba kwa sasa anatamba na wimbo wake mpya wa Seduce Me huku Diamond Platnumz akifanya vizuri na nyimbo zake kama Fire, Eneka, I miss u na ule mpya wa ‘Zilipendwa’ ambao  umeimbwa na wasanii wote wa WCB.

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents