Burudani

RECAP: Je, Harmonize kafikia level za Alikiba na Diamond?? (Video)

Bongofive kupitia kipindi chake pendwa cha RECAP & MANDO el_mando_tz amezungumzia kuhusu neno linalotrend la kuwa na BIG3 yani wasanii watatu wenye level sana.

Ameeleza kuwa kwa maoni yake na kwa fact atakazozitaja Tanzania hatuna BIG3 bali tuna BIG2 ya Alikiba na Diamond.

Amesema kuwa ameona watu wengi wakisema kuna BIG3 ya Diamond, Alikiba na Harmonize, Harmonize huwezi kumuweka kwenye za Diamond na Alikiba.

Amesema kuna sababu nyingi sana kuwa Harmonize hawezi kukaa kwenye level za Diamond na Alikiba kutokana na mafanikio yao kimuziki lakini pia nguvu Yao kwenye muziki pia.

Ukitaja Tuzo walizoshinda, Fanbase, Show walizotumbuiza, Collabo kubwa na muziki wao kufanya vizuri ndani na nje ya nchi.

Mbali na hilo biashara wanazofanya kwa sasa ikiwemo Lebo zao na pia Biashara za media, ni ngumu kumuweka Harmonize hapo.

Harmonize yupo level za Rayvanny, Marioo, Jay Melody , Nandy na wengine.

Unakubaliana na El_mando_tz kwa asilimia ngapi??

 

 

Host: El_mando_tz cameraman Samirkakaa

Bonyeza Link hapo chini kuona uchambuzi zaidi.

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents