Burudani

RECAP: S2Kizzy kufanya kazi na Rihanna, Wizkid ndio Producer bora wa muda wote?? (Video)

Bongofive Kupitia kwenye kipindi chake cha RECAP & MANDO El_mando_tz leo kamzungumzia Producer Zombie S2kizzy.

Anasema köa namna S2kizzy alivyotengeneza Hits nyingi inawezekana akawa Producer bora muda wote.

Anaongeza sio Hits tu bali hata kuingia kwenye tuzo za GRAMMY kunamfanya awe Producer wa Kipekee.

Kwa sasa kwenye game ya Bongofleva kwenye nyimbo 10 bora za mwezi utakutana na ngoma alizotengeneza yeye hata 8 au 7.

Kwa ufupi kwa sasa amelikamata Soko la Bongo Fleva inawezekana akiwa Majan Master Jay na wengine wamefanya makubwa lakini S2kizzy ana upekee wake mwa namna alivyotengeza Hits nyingi.

Unakubaliana na el_mando_tz kwa asilimia ngapi??

Uchambuzi mzima upo kwenye Akaunti yetu ya Youtube ya Bongofive.

 

 

Host:El_mando_tz Cameraman Samirkakaa

 

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents