Burudani

Rich Mavoko ajiteua balozi wa watoto waliofungwa jela!

Rich Mavoko amejiteua mwenyewe kuwa balozi wa watoto waliofungwa jela kwakuwa alipitia maisha hayo kipindi akiwa mdogo.

Rich Mavoko
Rich Mavoko

Rich amesema ameamua kuchukua uamuzi huo kutokana na jinsi watoto wanavyoweza kupoteza malengo yao pamoja na haki zao.

“Nataka nianze Dar es Salaam nikifanikiwa kuwatembelea na kuwapa baadhi ya mahitaji pamoja na kuwatia moyo nitaanza kutafuta na sehemu nyingine za Tanzania,|” ameiambia Bongo5.

“Kwahiyo nitakuwa kama balozi wao, ni maisha ambayo nimetokea ambayo yanafanana na wale, kwa sababu mimi nilishabadilika na sasa hivi muziki wangu unaweza ukanifanya hata nikizungumza nao na kuwapa ushauri wanaweza wakanielewa.

Kwahiyo mimi maisha hayo nimepitia ila sikufanikiwa kuingia kule ambako wao wapo lakini mimi maisha ya kulala lock up yalikuwa maisha ya kawaida. Tena ilikuwa haipiti wiki moja au mbili sijapelekwa. Hii kazi nimeiachia management yangu wanashungulikia kwahiyo soon tutaanza kufanya hilo zoezi kwa Dar es salaam.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents