Burudani

Rihanna na Shakira wawakera Waarabu, kwa kutangaza ‘usagaji’ kwenye video yao mpya

Kujizungusha kitandani na Rihanna huku wakivuta, Cigar, kumemweka Shakira kwenye maji ya moto.

Rihanna-and-Shakira-3095886

Hivi karibuni Shakira aliachia video ya wimbo wake “Can’t Remember to Forget you” aliomshirikisha Rihanna iliyoleta tafrani kubwa katika nchi za Kiarabu. Shakira ameshutumiwa kwa ‘kupromote usagaji’ na Rihanna kwenye video hiyo.

“Ni video ya kisagaji,” Fadi Haddad, muongozaji wa video wa Lebanon alikiambia kituo cha runinga Al Arabiya News.

Shakira, ambaye asili yake ni Columbia, analaumiwa zaidi kutokana na babu na bibi yake kuwa na asili ya Lebanon na walihama kutoka Lebanon kwenda New York City, ambako baba yake alizaliwa.

Video hiyo iliyowekwa kwenye mtandao wa YouTube, Jan. 31, iliangaliwa kwa zaidi ya mara milioni 88 ndani ya wiki moja pekee na sasa imeshaangalia kwa zaidi ya mara milioni 100.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents