Habari

RIPOTI: Vifo vya waandishi wa habari vyaongezeka duniani, Afghanistan ndio taifa lililoongoza kuua waandishi wengi kwa mwaka 2018

Leo Mei 3, 2019 ni siku ya kimataifa ya kusherehekea Uhuru wa Vyombo vya Habari duniani, ambapo kwa mujibu wa shirikisho la waandishi habari wa kimataifa (IFJ) limedai kuwa vifo vya waandishi wa habari duniani vimeongezeka hadi kufikia 95 kwa mwaka 2018.

Idadi hiyo ya vifo ipo juu zaidi ukilinganisha na idadi ilyotolewa na Shirikisho hilo ya mwaka 2017, ambapo waliuawa waandishi 81.

Takwimu hizi zinajumuishawaandishi wa habari wote duniani wanaofanyakazi kwenye mashirika ya shirika la habari.

Kiwango cha juu kabisa cha vifo vua waandishi wa habari kuwahi kutokea ilikuwa mwaka 2006 ambapo waandishi 155 waliuawa duniani kote.

VIFO VYA WAANDISHI WA HABARI VILIVYOTIKISA DUNIA MWAKA 2018:

1: JAMAL KASHOGI

Kifo cha mwandishi kilichoigusa dunia kwa mwaka 2018 kilikuwa ni cha mwandishi wa habari wa Saudia, Jamal Khashoggi. Aliuawa mwezi Oktoba ndani ya ubalozi wa Saudia nchini Uturuki.

2: AHMED HUSSEIN-SUALE

Ni mwandishi wa habari za upelelezi nchini Ghana alipigwa risasi hadi kufa wakati akiendesha gari kwenda nyumbani kwake, Na hii ilitokea siku chache baada ya mwanasiasa kumtishia kumdhuru.

Vyombo vya habari vya ndani viliripoti kuwa watu wasiojulikana wakiwa katika pikipiki walimpiga risasi Ahmed Hussein-Suale mara tatu katika mji mkuu wa Accra.

Alikuwa ni miongoni mwa wahusika wa shirika binafsi la upelelezi Tiger Eye na alipepeleza rushwa katika ligi ya mpira wa miguu Ghana.

JE, NI NCHI GANI DUNIANI IMEONGOZA KWA MAUAJI?

Afghanistan ndio nchi ilio hatari zaidi kuishi kwa mwandishi habari, ambapo waandishi 16 waliuawa mwaka 2019, ikifuatiwa na Mexico 11, Syria na Yemen 8, India 8 na Marekani waandishi watano.

ramani

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents