Burudani

Riyama asema mahusiano ya mapenzi hayaingiliwi, ni baada ya kuambiwa anapenda kutoka kimapenzi na vijana wadogo

Msanii wa filamu nchini Riyama Ally baada ya kuachana na baba mtoto wake ambaye alimzidi miaka 10, na hivi karibuni kutolewa mahari na msanii chipukizi wa muziki, Leo Mysterio ambaye pia amemzidi umri, watu mbalimbali katika mitandao ya kijamii wamekuwa wakihoji kwanini wanadada huyo anapenda kutoka na dogodogo.
IMGdd

Akizungumza katika kipindi cha Enewz cha East Africa Radio, Riyama amesema kuwa Leo Mystereo ndiyo furaha yake, na ujio wake katikia maisha yake umemuongezea changamoto kwenye maisha yake na kumfanya awe na furaha muda wote.

“Watu wanatakiwa wajue penzi haliingiliwi wewe ukicheka au ukinuna mimi hainisaidii kwani mimi natafuta furaha yangu na huyu ndiye furaha yangu, wewe unataka mimi niondoe furaha yangu nitaipata wapi. Unataka niwe na babu wa miaka mingapi ili uone Riyama ana heshima huyo babu unayetaka niwe naye asiponiheshimu pia mtasema. Jamani binadamu kweli maneno yapo kwa ajili ya kusema ila inabidi tuwe tunachagua vitu vya kusema,” alisema Riyama Ally.

Riyama alisema kuwa wapo baadhi ya watu wamekuwa wakiongea vibaya sana juu ya mahusiano yake lakini amewataka kutambua kuwa wao wamependana na wana mipango na wameridhiana wao hivyo kuwatenganisha kwa maneno si jambo jepesi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents